Kutoonekana kwa Kizz Daniel, chanzo ni begi la nguo

HomeKitaifa

Kutoonekana kwa Kizz Daniel, chanzo ni begi la nguo

Sababu zilizopelekea Kizz Daniel kutokupanda kwenye jukwaa la Summer ambalo huandaliwa na kampuni ya Sre8vibes kutoka nchini Tanzania zinadaiwa kuwa ni begi la nguo kusahaulika nchini Kenya.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa waandaji wa show hiyo wameieleza Bongofive kuwa, msanii Kizz Daniel alichelewa Ndege kutoka Nairobi nchini Kenya na ikabidi abadilishiwe Ndege kwahiyo akapata Ndege inayofuata.

kutokana na pressure ya kuchelewa Ndege zile haraka zikapelekea moja ya begi lake kusahaulika uwanja wa Ndege wa Jommo Kenyatta nchini Kenya.

Kizz Daneil alipofika Tanzania majira ya saa tatu kwenda saa nne usiku hakujua kama moja ya begi lake limesahaulika nchini Kenya uwanja wa Ndege na hiyo yote ni kutokana na pressure za kuwahi Tanzania.

Alipotoka Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwenda hoteli hakujua chochote mpaka alipofika hotelini ambapo walifikia Rotana Hoteli Post ndio akagundua kuwa begi moja ambalo lilikuw ana nguo zake za show limesahaulika Kenya.

Ikabidi afanye utaratibu wa kupata nguo zingine na kwakuwa usiku ulikuwa tayari umeingia na maduka yote yalikuwa yamefungwa ikabidi wamtafute mmoja ya msanii hapa Tanznaia ambaye ana ukaribu naye alipompigia ampatie nguo au designer wa Tanzania wanaojua kushona nguo msanii huyob alifanya hivyo lakini pia akampelekea na nguo zake azijaribu.

Nguo za msanii huyo zikaonekana ni ndogo kwa Kizz Daniel ikabidi watafute Designer wengi na msanii akawa anataka aina fulani tu ya nguo za show na inaelezwa alikuwa anataka full black na zile zilizoletwa na wabunifu kutoka Tanzania akawa hajazipenda.

Mvutano ulianzia pale msanii anataka aina fulani ya nguo na zile zingine zote anadai hakuzipenda na full black ya size yake haikupatikana kutokana na muda ulikuwa umeenda sana majira ya saa 10 alfajiri.

Baada ya msanii kuona vile na kwa ajili ya kulinda image yake na Brand mwisho ukawa msanii hataki kupanda jukwaani kisa nguu na begi lake la nguo limesahaulika Nairobi Kenya.

SOURCE : BONGOFIVE

 

error: Content is protected !!