Leo katika Historia: Mchoraji mashuhuri Pablo Picasso anazaliwa

HomeElimu

Leo katika Historia: Mchoraji mashuhuri Pablo Picasso anazaliwa

Siku kama ya leo mwaka 1881, alizaliwa Pablo Picasso mchoraji mashuhuri wa Hispania. Picasso alikuwa mwasisi wa harakati za Cubist ambazo zilienea kwa kasi kubwa miongoni mwa wachoraji wa Ufaransa.

Pablo Picasso alichora picha nyingi na daima alikuwa akifanya juhudi za kuendeleza harakati hiyo. Mchoro wa ‘The Girls of Avignon’ wa mchoraji huyo ndio uliokuwa mwanzo wa mtindo wa Cubism na kazi kubwa zaidi ya Picasso katika mtindo huo ni ‘Guernica’.

Katika mchoro huo Pablo Picasso anaonesha hofu iliyompata kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Ujerumani na Italia dhidi ya mji wa Guernica. Picasso alifariki dunia Aprili mwaka 1973.

error: Content is protected !!