Ijue maana ya nyota yako leo Oktoba 25, 2021

HomeNyota

Ijue maana ya nyota yako leo Oktoba 25, 2021

NDOO(Jan 21- Feb 19):ni kipindi cha kutoa maamuzi kwani mambo mengi uliyopanga yatakwamuka, hutarudi nyuma na furaha itatawala kwa maamuzi yako. Tumia muda mwingi kuwa na familia yako.

SAMAKI(Feb 20- Machi 20):unahutaji ushindi, lakini kuna changamoto nyingi zinajitokeza katika kufikia lengo lililokusudiwa. Kuwa mwangalifu katika kukwamua mambo yako ya msingi.

KONDOO(Machi 21- Aprili 20):hutakuwa na uchovu baada ya mapumziko ya kutosha kutokana na wingi wa mambo yalivyokuzonga. Jenga tabia ya kuwa karibu zaidi na rafiki zao wa karibu.

NG’OMBE(April 21- Mei 21):katika kipindi hiki kuwa karibu na marafiki ambao watatoa mchango kubwa katika mafanikio yako kwa kuwa mambo yako mengi yataweza kukamilika kama ulivyopanga.

MAPACHA (Mei 22- Juni 21):mpango wako wa kuelekea katika eneo jingine la kazi ulilokuwa ukitarajia kwa muda mrefu litakamilika.Jiandae na mambo yako ya msingi yajayo na achana na tabia ya kukurupuka hasa katika kutoa maamuzi ya haraka.

KAA(Juni 22- Julai 22):utakuwa ni mwenye kufuatiliwa na wengi katika siku za hivi karibuni. Hawatafanikiwa kwa waliokuandalia ambalo yanaonekana kuwa linaweza kuwa na athari baadae.

SIMBA(Julai 23- Aug 23): ijapokuwa maamuzi yako sio sahihi, pia utajuta kwa kugundua kuwa hutaweza kukamilisha mambo yako mengi kwa wakati uliopanga. Kuwa na msimamo imara ni sehemu ya mafanikio.

MASHUKE(Aug 24- Sept 23): licha ya kwamba ukovyema katika kushughulikia mambo mengi sio tu yanayokwamisha mipango ya maisha yako bali pia mpenzi wako pamoja na marafiki , watu wanapenda kuwa nawe karibu hasa kwa jinsi unavyowapa matumaini na  kuwajali.

MIZANI(Sept 24- Okt 23): ni kipindi cha mafanikio makubwa katika sehemu yako ya kazi na kila uliloluwa ukitarajia kwa muda mrefu litazaa matunda ya mafanikio lakini pia jenga utamaduni wa kusaidia wengine.

NGE(Okt 24- Nov 22):jitahidi kupanga mipango yako ya muda mfupi ambayo utaweza kuitekeleza kwa wakati, kuliko kuwa na wingi wa mipango ya muda mrefu ambayo kukamilika kwake haitakuwa rahisi.

MSHALE(Nov 23- Dis 21): kile unachokiamni leo ni tofauti na kile cha jana,halii hii huweka wakati mgumu kwa wengine kuweza kuungana nawe. Jaribu kuwa na mwendelezo kila inapowezekana.

MBUZI(Dis 22- Jan 20):kuwa mwenye zaidi kusikiliza mambo kuliko kuwa msemaji, hali ambayo itawavutia wengi na mchanganuo wa mawazo yako.

 

error: Content is protected !!