Lesotho yajifunza kutoka Tanzania kuhusu usimamizi wa nishati

HomeKitaifa

Lesotho yajifunza kutoka Tanzania kuhusu usimamizi wa nishati

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Lesotho, Bwana Tonkiso Phapano, ameongoza ujumbe maalum nchini Tanzania kwa ziara ya kimafunzo kuhusu usimamizi wa sekta ya nishati, hususan mafuta na gesi asilia.

Bwana Phapano alisema wamevutiwa na mfumo wa Tanzania, hasa baada ya wasilisho la Mission 300, na kuona ni mfano bora kwa maboresho ya sheria za nishati nchini mwao.

Ujumbe huo ulitembelea TPDC na kupata maelezo ya kina kuhusu shughuli zake. Kwa upande wake, TPDC kupitia Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bwana Derick Moshi, ilieleza utayari wa kushirikiana na Lesotho kubadilishana uzoefu na maarifa.

Moshi alibainisha kuwa TPDC inaendesha shughuli zake kupitia idara mbalimbali na kampuni tanzu mbili: GASCO kwa mitambo ya gesi asilia na TANOIL kwa biashara ya mafuta. Pia alieleza kuwa gesi asilia inayopatikana nchini inatumika kwa matumizi ya nyumbani, viwandani, na kuzalisha umeme.

error: Content is protected !!