Lissu: Serikali ibane matumizi

HomeKitaifa

Lissu: Serikali ibane matumizi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo , (Chadema) amesema sababu ya kupanda kwa gharama za maisha nchi ni kodi ambazo serikali imeziweka zinazolipwa na wananchi.

Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema kwamba wananchi wamebebshwa mzigo mkubwa wa kodi na njia pekee ni kwa serikali kubana matumizi.

“Wananchi wamebebeshwa mzigo wa kodi ajabu za kila aina, na kikatiba na kisheria hizo kodi zote zinaanzia kwa Rais zinaishia kwa Rais…kama inaambia watu wabane matumizi ibane matumizi,”

Alisisitiza pia, “serikali ibane matumizi ipinguze mzigo wa kodi kwenye bidhaa muhimu, hizi ambazo zinafanya maisha hayawezekani mtaani, kwa mfano kodi kwenye bidhaa zote za chakula,” amesema Lissu.

 

error: Content is protected !!