Lita 910 zingine za dizeli SGR zakamatwa

HomeKitaifa

Lita 910 zingine za dizeli SGR zakamatwa

Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema wamefanikiwa kukamata lita 910 za mafuta aina ya dizeli yanayotumika katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Pia amesema wamakamata pikipiki nane zilizokuwa zikitumika kwenye usafirishaji wa mafuta hayo.

Kamanda Magomi amesema operesheni ya kusaka wizi huo imefanyika kwa muda wa wiki mbili.

Jana Jeshi la Polisi mkoani Mwanza lilitangaza kukamata lita 850 za mafuta ya dizeli na watuhumiwa wanne wanaodaiwa kufanya makosa likiwemo la wizi wa vifaa yakiwamo mafuta katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

error: Content is protected !!