Lugha 5 za mapenzi wanazopenda wanawake zaidi

HomeElimu

Lugha 5 za mapenzi wanazopenda wanawake zaidi

Miezi ya mwanzoni katika mahusiano huwaga ya furaha na mara nyingi ni ngumu sana kuona makosa ya mwenzi wako, Lakini mnapokaa muda mrefu kwenye mahusiano mambo hubadilika, wanasema mapenzi yanaisha yanabaki mazoea. Ili uweze kudumu kwenye mahusiano hayo unahitaji kujua lugha gani ya mapenzi unaweza kutumia kwa mwenzi wako.

Gary Chapman aliandika kitabu kinachoitwa lugha tano za mapenzi yaani “The five love languages” ambazo ni kama zifuatazo

Zawadi
Lugha hii ya mapenzi wanawake wengi ndio wanaipenda, yaani ukiwa na mpenzi wako na ukawa unamnunulia zawadi mbalimbali kama saa, manukato, nguo na maua anahisi kuwa hayo ndo mapenzi. Kila mara utakapokua unafanya hivyo ndivyo atajisikia vizuri zaidi na yeye kuzidisha upendo kwako kwani ameona anapendwa.

Muda
Pamoja na kwamba kuna majukumu unapaswa kuyatimiza nje ya mahusiano yako lakini kwa uhai wa mahusiano yako unahitaji kutenga muda kwaajili ya mpenzi wako, watu ambao mapenzi kwao ni kupewa muda wanategemea kuona unamzingatia kwenye kila uanchokifanya kama kutoka nae na kumpeleka sehemu akaangalie sinema, kula, kuangalia wanyama au hata kwenda matembezi ya usiku lakini pia kuwa nae siku muhimu kama sikukuu mbalimbali au kipindi cha mapumziko.

Kumsaidia kazi
Kumsaidia mpenzi wako kazi ni njia moja wapo pia ya kuwasiliana nae na kumuonyesha kuwa unampenda, hii ni kwa wote mwanaume anaweza akafanya hata mwanamke kazi kama kuchota maji, kusafisha nyumba, kufua kuogesha na kuvalisha watoto na majukumu mengine ambayo unaweza kumsaidia mpenzi wako.

Maneno ya Uthibitisho
Kama mpenzi wako anatabia ya hofu basi ni vizuri kutumia lugha ya uthibitisho kumuonyesha kuwa unampenda, unaweza kumthibitishia unampenda kwa kumwambia mara kwa mara kuwa unampenda lakini pia kwa kumtumia jumbe za mapenzi pamoja na kadi zenye ujumbe wa kuonyesha unampenda na kumuhitaji.

Kushikwa
Lugha ya mapenzi ya kushika inahusisha kushikwa kwa mahaba kama kukumbatia, kumbusu, kumtekenya na kufanya nae mapenzi, mpenzi wako akiwa anapenda hivyo mfanyie huku ukimaanisha na sio kumridhisha. Kumbuka lugha hizo sio kila mtu anazipenda hivyo ni vyema kumjua mpenzi wako na lugha ipi au zipi zitamfaa, zipo nyingine ambazo sio wengi wanaozipenda kama lugha ya ishara kama kutabasamu na kukonyeza au mtindo wa maisha wa mtu kama kuwa na nyumba ya kifahari, kuvaa nguo za bei ghali na maeneo gani anapenda kuishi na kutembea.

error: Content is protected !!