Soda ni moja ya vinywaji pendwa sana kwa watoto, wazee na hata vijana lakini ni kati ya kinywaji hatari sana katika mwili wa binadamu kwani madhara yake ni makubwa na kwa kiasi kikubwa inahusika na uharibifu wa kinga ya mwili.
Katika kulitambua hilo tumekuwekea hapa madhara 8 yatokanayo na unywaj soda.
1.Kupungua kwa madini mwilini
Kinywaji hiki pendwa kina Kemikali inayoitwa “Phosphoric acid” ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya chokaa kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli.
2.Kubadilika kwa rangi ya meno
Kama unasumbuliwa na tatizo la meno basi ni wakati sasa uache kunywa soda kwani tindikali iliyopo ndani ya soda hubadili rangi ya meno.
3.Huzeesha
Siku hizi ni kawaida kukutana na kijana mwenye miaka 20 kuonekana kama ana miaka 35 na hii ni kwa sababu ya matumizi ya soda kwa wingi.
4.Kupungua kwa maji mwilini
Soda ina madini mengi ya sodium ambayo yanakausha maji mwilini hivyo unywaji wa soda unakufanya uwepo kwenye hatari ya kupungukiwa kwa maji mwilini tatizo lilaloweza kumletea shida za kiafya kwenye Figo na Nyongo.
> Madhara 8 ya kuchora “Tattoo” mwilini.
5.Kitambi, Kitambi, Kitambi
Tafiti zinazoonesha mnywaji wa soda hunenepa mara 2 zaidi ya mtu asiyekunywa soda na yupo katika uwezekano mkubwa sana kupata kitambi pamoja na kuongezeka uzito.
Ongezeko la sumu mwilini
Kimsingi kabisa, soda sio lishe, hivyo ukiwa mpenzi wa kinywaji hiki basi tambua kuwa unaongeza sumu mwili mwako na kujitengenezea matatizo makubwa ya kiafya.
7.Ugonjwa wa kisukari
Kumbuka kuwa soda 1 ni sawa na kula vijiko 10 vya sukari, hivyo endapo utakuwa mnywaji sana wa soda kuna uwezekano wa kongosho lako kushindwa kufanya kazi vizuri.
8.Kufa kwa seli za Ubongo
Unywaji wa soda huleta shida kwenye Ubongo na ndio maana mara nyingi unakuta mtu anakua na usahaulifu wa mambo, kiharusi na matatizo mengi ya Ubongo.
Ni vyema mtu ukanywa maziwa freshi ya Ng’ombe, Juisi ya kutengeneza nyumbani na maji ili kulinda mwili wako dhidi ya maradhi hayo. #clickhabari