Kuna raha ya kuoga maji ya moto , hasa ukiyapata usiku au mchana baada ya kazi ngumu na mihangaiko chini ya jua kali. Lakini je, ni kwa kiasi gani ngozi yako inaweza kuhimili maji hayo? Wapo watu ni mtindo wa maisha yao kuoga maji ya moto kila siku, iwe mchana au usiku. Lakini licha ya raha mtu anayoweza kupata kutokana na maji hayo, lakini kupendelea sana kutumia maji hayo inaweza kuwa na athari kwenye ngozi ya mwili wako.
Hata kama ni mraibu wa kipindi kirefu wa kuoga maji ya moto na hujawahi kupata madhara yeyote ya ngozi, haina maana kuwa maji ya moto ni salama kwa ngozi yako.
kuoga maji ya moto ni kweli utajisikia vizuri unapooga lakini kunaharibu ngozi yako hivyo fahamu madhara yatokanayo na kuoga maji ya moto mara kwa mara:
1. Kuharibu seli za ngozi
Ngozi ya mwanadamu inaundwa kwa matabaka matatu, kama unapendelea kutumia maji ya moto kwa kuogea una hatari ya kuathiri tabala la juu linaloitwa epodermis. Zipo chembe hai (seli) zinazoitwa keratin cells ambazo zinapatikana kwenye tabaka la juu la ngozi ya mwanadamu, kazi kubwa ya seli hizi ni kutunza unyevunyevu ndani ya ngozi ya mwanadamu hivyo pindi zinapopata joto la maji mara kwa mara huaribika na kuleta athari kwenye ngozi ya mtu.
> Jifunza namna bora za kuzuia na kutibu chunusi
2. Husababisha mikunjo kwenye ngozi
Mfululizo wa kuoga maji ya moto husababisha mafuta yaliyopo kwenye ngozi kukauka na kusababisha mikunjo. Joto maji likichanganyika na sabuni hulainisha ngozi yako na kuiweka katika mazingira hatarishi ya kusinyaa na kukauka.
3. Inaweza kukuleta magonjwa ya ngozi
Maji ya moto yanazibua vitundu vya hewa vilivyopo kwenye ngozi na kuiacha ngozi kuwa wazi, ngozi yako inapokua wazi ni rahisi sana kushambuliwa na Bakteria na kusababisha magonjwa mbalimbali ya ngozi kama vipele na miwasho.