Majaliwa: 2025 ni Rais Samia

HomeKitaifa

Majaliwa: 2025 ni Rais Samia

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama cha Mapinduzi kitampeleka Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi.

Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa ajili ya Mawaziri na Manaibu Mawaziri leo jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wateule hao wa Rais kutambua kwamba kwa kuwa Rais Samia ndiye atakayepelekwa kwa wananchi mwaka 2025 na hivyo wawe wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali

Amesema “Waambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza,”

          > Wakurugenzi dhaifu kupelekwa kwa Rais Samia

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Mawaziri na Manaibu wao kuwa mfano na kielelezo katika miendeno yao wakianz ana mavazi na kauli zao.

Pia amewatka kutojihusisha katika mijadala au yasiyofaa kwa lengo la kuwafanya wazungumziwe, na kuhakikisha kwamba hawaongei mambo mengi mtandaoni ili yale machache wanayoongea yaonekane kuleta matokeo.

Mwaka 2025 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, ambapo kwa kauli iliyotolewa leo na Waziri Mkuu inaashiria kwamba Chama Cha Mapinduzi kinakusudia kumsimamisha Rais Samia Suluhu Hassan kama mgombea wa kiti cha Urais.

error: Content is protected !!