Majasusi wa Urusi wahusishwa na wizi wa ‘formula’ ya chanjo Uingereza

HomeKimataifa

Majasusi wa Urusi wahusishwa na wizi wa ‘formula’ ya chanjo Uingereza

Vyanzo vya habari vya Uingereza vimekuwa vikieneza uvumi kuwa Urusi imeiba njia (formula) ya kutengeneza chanjo aina ya AstraZeneca na kutengeneza chanjo yake aina ya Sputnik V.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavron amesema kuwa madai hayo hayana ushahidi na ameomba yapuuzwe kwani yana lengo la kuichafua Urusi.

Oktoba, 10 Gazeti la ‘The Sun’ la nchini Uingereza lilitangaza kuwa majasusi wa Urusi wameiba ‘formula’ ya kutengeneza chanjo ya Oxford-AstraZeneca ambayo huzalishwa kwa ubia wa Uingereza na Sweden na kuzalisha kutengeneza chanjo ya Sputnik V.

Waziri huyo wa Urusi amesema kuwa “kumekuwa na kesi kadhaa juu ya watu kuganda damu baada ya kutumia AstaZeneca, lakini haijawahi kutokea hivyo kwa Sputnik V, kwa mtu mwenye uelewa atahimitimisha mwenyewe kwenye hilo na kujua ukweli ulipo.” Amesema Lavron

error: Content is protected !!