Majengo marefu Zaidi Afrika 

HomeBiashara

Majengo marefu Zaidi Afrika 

Historia ya majengo marefu barani Afrika ilianza mwaka 1973 baada ya ujenzi wa jumba refu la Carlton Centers jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambalo lilishikilia taji la jumba refu Zaidi barani Afrika mpaka Aprili2019 kwa takwimu za mtandao wa CK.

Katika Makala hii tutaangazia baadhi ya majengo marefu zaidi Afrika kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa CK.

1. The Leonardo | Sandton
Jengo hili linapatikana Afrika kusini lina urefu wa mita 227 ikiwa na ghorofa 56. Jengo hili linapatikana barabara ya 75Maude, takribani mita 100 kutoka katika jumba la hisa la Johannesburg Stock Exchange.
Mtandao wa CK unaelezea kwamba ujenzi wa jumba hilo ulianza Novemba 17, 2015 na lilishika nafasi ya kwanza na kuongoza kuanzia mwaka 2019.

 

2. Carlton Centre
Carlton Centre, lina urefu wa mita 223, ni kituo kikuu cha maduka tofauti mjini Johannesburg na limekuwa jumba refu barani Afrika kwa muda mrefu kabla ya ujenzi wa jumba la Leonardo.

3. Britam Tower
Jengo hili linapatikana jijini Nairobi nchini Kenya, lina urefu wa mita 200 na limejengwa katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi. Lilifunguliwa rasmi mwaka 2018, na kulipiku jumba la UAP Old Mutual kama jumba refu zaidi nchini Kenya, likiwa na ghorofa 31.

4. Commercial Bank of Ethiopia ‘CBE’
Jengo la makao makuu ya CBE yaliyopo nchini Ethiopia lina urefu wa mita 198 na linamilikiwa na Benki ya Biashara ya Ethiopia (Commercial Bank of Ethiopia ‘CBE’). Lipo katikati ya mji wa Addis Ababa.

5. Nairobi GTC Office Tower.
Jengo hili linapatikana nchini Kenya katika jiji la Nairobi, GTC Office Tower, ambalo ndio jumba refu kati ya majumba sita ya Global Trade Centre. Jumba hilo lina urefu wa mita 184 na ghorofa 43, ndilo linalotarajiwa kuwa makao makuu ya kampuni ya China ya Avic ambayo inataka kujikita katika eneo la Westland mjini Nairobi.

6. Ponte City
Jumba la Ponte City lina urefu wa mita 172.8, lipo katika makazi ya mji wa Johannesburg Afrika Kusini. Likiwa limejengwa 1975, jumba hilo lenye ghorofa 54 limetajwa kuwa jumba la kwanza la mviringo kujengwa Afrika.

7. UAP Tower
Jengo hili lipo nchini Kenya katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi, lina urefu wa mita 163. Liliwahi kuwa jengo refu zaidi Afrika Mashariki lilipofunguliwa mwaka 2016.

8. NECOM House.
Jumba hili lililopo nchini Nigeria, kwa mujibu wa mtandao wa CK, jumba la NECOM lililojulikana kama NITEL Tower na awali The NET Building, lina urefu wa mita 158 katikati ya mji wa Lagos.

Ndilo jumba refu lililo rasmi nchini Nigeria eneo zima la Afrika Magharibi. Jumba hilo lililokamilika 1979 ndio makao makuu ya kampuni ya NECOM Telecommunication Ltd iliyokuwa ikimilikiwa na serikali.

9. Tanzania Ports Authority Tower.
Jumba la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), lina urefu wa mita 157, lipo katika mji wa kibiashara wa Dar es Salaam. Baada ya ujenzi wake kukamilika mnamo mwaka 2016, jumba hilo lenye urefu wa mita 40 ndio makao makuu ya shirika la Bandari nchini Tanzania.

10. PSPF Towers.
Jengo lililopo Dar es Salaam nchini Tanzania. Jengo la PSPF Towers lina urefu wa mita 153 na linatumika kama ofisi.

error: Content is protected !!