Makosa 5 yakuepuka wakati wa kununua gari

HomeBiashara

Makosa 5 yakuepuka wakati wa kununua gari

Kumiliki gari ni kitu ambacho watu wengi wanatamani kutokana na adha ya usafiri hasa jijini Dar es Salaam ambako wingi wa watu unafanya usafiri wa umma kuwa na changamoto nyingi, zikiambatana na hatari ya kuambukizana magonjwa na wizi.

Lakini unapofikia uamuzi wa kununua gari, kuna mambo ya msingi unayotakiwa kuzingatia ili hata unapotaka kuliuza gari hilo ununue ama toleo jipya au gari jingine, basi usipate changamoto sana kupata mteja. Baadhi ya mambo yanayopuuziwa na mwishoni humgharimu muuzaji wa gari ni;

1. Gharama za matengenezo ya gari unalotaka kununua ikiwa pamoja na gharama za mafuta ya gari. Gharama za matengenezo ya gari hupanda mwaka hadi mwaka kutokana na huduma mbalimbali zinazohitajika kufanyika kwenye gari hilo kwani kadri siku zinavyoenda ndivyo matengenezo ya gari yanakuwa makubwa.

2. Kununua toleo jipya la gari. Haishauriwi sana kununua toleo jipya la gari, kwa sababu baadhi ya matoleo hutengenezwa na kuyapa muda wa majaribio ili kufanya maboresho katika toleo lijalo, hivyo inashauriwa kununua magari yaliyotoka miaka mitatu iliyopita.

3. Tambua wakati wa kununua. Sio kila mwezi ni wa kununua magari, inashauriwa miezi mizuri ya kununua gari ni kuanzia mwezi wa 12 mpaka mwezi wa 3 ili kuokoa kiasi cha pesa kwani miezi hii kampuni mbalimbali zinazouza magari hutoa ofa ya kushusha bei ili kuuza bidhaa zao.

4. Fikiria kuhusu mauzo ya gari lako pindi utapotaka kuliuza ili ubadilishe gari jingine. Hapa kikubwa kinachoangaliwa ni jina la gari, kuna magari magumu sana kuingia sokoni na kununulika kutokana na upatiakanaji wa vifaa vya ziada pindi gari hilo linapokuwa limeharibika, pia inashauriwa kuzingatia rangi ya gari lako ambapo watu wengi hupendelea gari rangi nyeusi, fedha na nyeupe.

5. Jambo la mwisho. Usiwe na haraka ya kununua gari, fanya tafiti sehemu mbalimbali, watumie watu wanaojua juu ya magari wakushauri juu ya gari unalotaka kununua kusanya taarifa sahihi kisha fanya maamuzi, usikurupuke.

error: Content is protected !!