Mahakama yamwachia huru Rugemalira

HomeKitaifa

Mahakama yamwachia huru Rugemalira

 

Mahakama ya Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo Septemba 16, 2021 imemwachia huru James Rugemalira baada ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali kufuta mashitaka 6 ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yanamkabili tangu 2017.

Mshitakiwa mwezak, Seth Habinder aliachiwa huru baada ya kulipa shilingi milioni 200 kati ya bilioni 26 ambazo anatakiwa kulipa, huku kiasi kilichobaki kitalipwa taratibu ndani ya miezi 12.

Harbinder Seth Sign na James Rugemarila walishitakiwa tangu 2017 kwa kesi uhujumu uchumi. Wote wawili walihusika kwenye sakata ya Tegeta Escrow ambapo kwa mara ya kwanza walisomewa mashitaka ikiwamo kutakatisha fedha, kughushi nyaraka, ufisadi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu ambapo walisababisha upotevu wa shilingi bilioni 309.

error: Content is protected !!