Maji yaanza kujazwa bwawa la Julius Nyerere

HomeKitaifa

Maji yaanza kujazwa bwawa la Julius Nyerere

Historia imeandikwa leo nchini baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kubonyeza kitufe cha kuruhusu maji kujaa katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere(JNHPP) na kuashiria upatikanaji wa suluhu ya tatizo la umeme kwa Watanzania.

Katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo ulibebwa na kauli mbiu ya “Bwawa letu, bwawa lako, bwawa langu”, Rais Samia amewataka wananchi na viongozi wote kwa ujumla kuhakikisha wanakuwa wazalendo na kulinda mradi huo unaotarajiwa kuwa kichecheo kikubwa cha uchumi nchini.

“Kauli mbiu ya ‘Bwawa letu, bwawa lako, bwawa bwawa langu” Ni kauli mbiu ambayo inatuunganisha kama Taifa na kudhihirisha umoja na uzalendo katika kulinda mradi huu,” amesema Rais Samia.

Pia, amesisitiza kwamba maelekezo yaliyotolewa na Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango kuhusu utunzwaji wa mazingira na uondoaji wa mifugo katika maeneo ya hifadhi yafuatwe ili mazingira yaendelee kuwa rafiki.

error: Content is protected !!