Mabaki ya mijusi mikubwa (Dinosaurs) yana faida kubwa sana kwa Taifa, mbali na faida ya uchumi inayofahamika sana na ambayo yaweza kuwa ndio faida ya mwisho.
Mabaki ya mijusi hii ni alama ya maisha ya kale na inatujuza juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya tabia ya ardhi na namna gani viumbe vya kale viliweza kuhimili au kuishi kulingana na mabadiliko yote hayo. Mifupa ya mijusi iliyogunduliwa na jopo la watafiti Tendaguru mkoani Lindi, inasemekana ni ya mijusi iliyoishi eneo hilo miaka milioni 150 iliyopita.
Haya ni mambo 10 kuhusu mabaki ya mifupa hiyo
1. Neno ‘Tendaguru’ limetokana na lugha ya kabila ya kimatumbi ‘Tendagulu’ lenye maana Ukungu unaotanda asubuhi kutokana na baridi.
2. Kipo kitabu maarufu cha kiswahili cha watoto kilichondikwa na Watanzania Cassian Magori na Charles Saanane kinachoitwa Dinosaria wa Tendaguru kilichochapishwa 1998.
3. Mabaki ya kwanza ya mifupa hiyo yalianza kuchimbwa kati ya 1906-1913
4. Mabaki ya kwanza kungundulika yalikuwa na uzito wa tani 230 na yaliyogunduliwa tarehe 2 Oktoba 2021 yana uzito wa tani 2.
>Madhara 8 ya kuchora “Tattoo” mwilini.
5. Mabaki ya mjusi ya Tendaguru yamehifadhiwa katika makumbusho ya Berlin nchini Ujerumani
6. Mabaki yaliyochimbwa yanaonesha mjusi huyo alikuwa mkubwa mara 3 zaidi ya tembo mkubwa.
7. Tendaguru ni eneo muhimu zaidi la ugunduzi wa mifupa hiyo duniani.
8. Mifupa ya mjusi wa Tendaguru iliyounganishwa na kupata umbo kamili la mjusi nchini Ujerumani, ina urefu mita 14 na ndio mjusi mkubwa wa maonesho kuliko yote duniani.
9. Mwaka 2018 Serikali ya Tanzania ilianza mazungumzo ya awali na Serikali ya Ujerumani kuona namna gani wanaweza kugawana faida inayopatikana kutokana na mjusi huyo.
10. Yuko mjusi wa Tendaguru anayeitwa ‘Nyorosaurus’ ambaye jina lake linatokana na mtanzania Seliman Nyororo ambaye alikuwa kinara kwenye kuwaelekeza watafiti wa Kijerumani eneo ambalo mabaki ya mjusi huyo yanapatikana.