Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete

HomeElimu

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete

Katika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo Oktoba 7, 2021, kila mtu ameonesha hisia zake katika kusherehekea siku hiyo kwa namna anayoona yeye inafaa.

Lakini Clickhabari tumeona sio vibaya tukikuletea mambo 10 yanayomhusu Dkt. Kikwete, kuanzia maisha yake ya utotoni, uongozi katika ngazi mbalimbali serikalini hadi kustaafu, ambayo pengine huyafahamu.

1. Alipata viatu vyake vya kwanza ‘Raba’, alipotoka jandoni. Alipokwenda shule na viatu vile, mwalimu alimkataza asivivae tena shuleni kwani shule nzima hakuna mwenye viatu.

2. Mwaka 1994, akiwa na umri wa miaka 44, aliwahi kuwa Waziri wa Fedha, ndio mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwa waziri katika wizara hiyo.

3. Katika historia ya Tanzania, Kikwete ndio waziri wa mambo ya nje aliyehudumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka mingi (miaka 10) kuliko waziri mwingine yeyote.

4. Dkt. Kikwete ana shahada za heshima kutoka kwenye vyuo vikuu 11, saba kati shahada hizo zikiwa ni za udaktari wa heshima.

5. Ipo miundombinu nane Tanzania yenye jina la Dkt. Kikwete (Daraja la Kikwete lenye urefu wa mita 275 katika mto malagarasi, viwanja vya michezo vya Kikwete Dar es Salaam, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Barabara yenye Km 12 Ilala hadi Chamazi, Dar es Salaam, Shule Msingi Kikwete Muleba Kagera, Shule ya Sekondari Kikwete Mbulu Manyara, Shule ya J.K Kikwete Mbozi Mbeya.

6.  Kikwete amezaliwa siku moja na watu mashuhuri kama Vladmir Putin, Diego Costa, Trent Alexander Arnold, Simon Cowell na Desmond Tutu.

7. Ni mpenzi sana wa mchezo wa kikapu, alishawahi kuwa kiongozi katika chama cha mpira wa kikapu Tanzania.

8. Jakaya Kikwete ni Mwanajeshi, alikwenda mafunzo ya kijeshi kati ya 1976 – 1976 na alipanda kufikia cheo cha Luteni Kanali.

9. Dkt. Kikwete aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU).

10. Dkt. Kikwete amehusika kwenye majadiliano ya amani katika za Burundi, Komoro, Congo DRC, Kenya, Madagascar, Zimbabwe na Libya.

error: Content is protected !!