Mambo 4 ya kufanya baada ya tendo la ndoa

HomeElimu

Mambo 4 ya kufanya baada ya tendo la ndoa

Unafahamu kwamba kuna mambo unatakiwa kufanya mara baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa? Ni muhimu kufanya hivyo hili kukuwezesha kubaki na afya salama.

Zinfatia mambo haya 4 mara baada umalizapo kushiriki tendo la ndoa.

Hakikisha unapata haja ndogo

Hakikisha unaenda kupata haja ndogo mara baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa hasa kwa wanawake kwani hii inasaidia kuondoa bakteria yoyote aliyeingia wakati wa kujamiana na pia kukupunguzia uwezekano wakupata magonjwa kama UTI.

Osha sehemu za siri vizuri

Humalizapo kushiriki tendo la ndoa hakikisha unaenda kunawa na kusafisha sehemu zako za siri kwa maji masafi. Husitumie sabuni kwani zinaweza kukufanya ukapata miwasho. Pia pindi ufanyapo hivyo hakikisha hausugui hasa wanawake kwani unaweza ukasababisha uvimbe katika maumbile yako.

Angalia kama umeumia au kuna alama za damu

Hakikisha unajiangalia kama umechubuka au kuna alama zozote za damu kwani vitu hivyo vinaweza kutokea wakati wa tendo na mtu asiweze kujua, na pindi ukiona umeumia au kuna uchafu ambao sio wakawaida unatoka basi nenda ukapate huduma haraka.

Chunguza kondomu

Mwisho kabisa angalia kondomu mliyotumia kama ipo sawa, ichunguze kama imepasuka au kama imezama kwenye sehemu za siri za mwanamke.

error: Content is protected !!