Unapofikia umri wa balehe wazazi na jamii wanajaribu kukulinda dhidi ya changamoto mbalimbali za ukuaji zinazotokana na mahusiano, Katika kipindi hiki ndipo wengi wanatamani kuwa katika mahusiano lakini pia kushiriki tendo la ndoa hivyo kuna baadhi ya uongo wanatuaminisha ili tuwe salama nao ni;
1. Utapata mimba ukiguswa na mwanaume
Hii ni mara nyingi inatokea kwa mabinti wa kike ambao wameanza kupata mabadiliko katika mwili, Mabadiliko ambayo wanaweza kupata hedhi kwa mara ya kwanza, kuota matiti na kuanza kuwa na shepu nzuri. Katika kipindi hichi kila mwanaume anaemuona anatamani kumtongoza na kushiriki nae ngono hivyo, ili kukuwekea wasiwasi na usifanye ngono utaambiwa usimsogelee au kukaa na wanaume utapata mimba lakini kadri unavyokua unajua kua ni uongo.
2. Muda wa kukubali kuanzisha mahusiano
Wengi wameaminishwa kwamba kama mwanaume ili apate mwanamke anaefaa basi lazima mwanamke huyo amtongeze kwa muda mrefu, Ikiwa mwanamke anaemtongoza atakubali haraka basi hafai ni sawa pia na kwa wanawake hawezi kukubali kuwa na mahusiano na mwanaume kwa haraka lazima amzungushe.Lakini ukweli ni kwamba amna muda maalum ambao mtu akikuzungusha kwa muda huo ndio atakua mtu sahihi kwako hapana ila tu kama haukuwa na upendo wa kweli inapotokea unazungushwa sana unaweza kukata tamaa.
3. Kufanya ngono siku ya kwanza kukutana
Hadi sasa bado nadharia hii imebaki kwenye vichwa vya watu wengi kwamba ikitokea umekutana na mwanaume au mwanamke siku ya kwanza, mkafanya ngono siku hiyo hiyo basi huyo mwanamke au mwanaume ni muhuni jambo ambalo sio kweli hiyo haibadilishi tabia ya mtu. Hata kama mtafanya ngono miezi mitatu au minne baadae baada ya kuwa mmekutana mara kwa mara.
4. Mwanaume hashikwi
Mbali na kuambiwa na wazazi kwaajili ya usalama lakini wengine kutoakana na tamaduni hawaruhusiwi kumshika mwanaume, Mwanamke hata kama anahitaji kuwa karibu na mpenzi wake au kumuandaa kwaajili ya tendo la ngono ila kwa sababu yeye ni mwanamke hawezi kumshika. Mambo yanabadilika sasa mwanaume anahitaji pia faraja na kujisikia vizuri unatakiwa ubadilike.
5. Mwenza wa roho
Watu wanaamini kwenye mahusiano mtu mmoja tu ndio ameumbwa kwaajili yao siku zote, Sio kweli ikitokea mambo hayajaenda sawa kwenye mahusiano uliokuwepo si lazima kuendelea kubaki hapo achana nae katafute mtu sahihi kwa ajili yako.