Furaha ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu lakini watu wengi tumekua tukijisahahu na kufanya mambo yanayotuondolea furaha maishani.
Unaweza usijue kwamba unatenda kitu kinachokuendolea furaha, yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayokuondolea furaha katika maisha yako.
Kulalamika sana
Mtu mwenye furaha hawezi kulalamika mara kwa mara kwani anapoona jambo halipo sawa siku zote hutafuta namna ya kutatua changamoto hiyo lakini ni tofauti na mtu asiye na furaha.
Kujutia yaliyopita
Watu wengine wanakosa furaha katika maisha yao sababu wanaishi kwa kulaumu yale yaliyopita na hii umfanya akosea hata amani na kusonga mbele.
Unachotakiwa kufanya ni kwamba sahau yaliyopita, usijilaumu na pia hakikisha kosa alijirudii tena.
Kuhofia ya mbeleni
Usiishi kwa kuhofia mambo ya mbeleni kwa kuwa wakati wake utafita na utafanya lile linalotakiwa kufanyika lakini kwa sasa ishi kwenye wakati uliopo.
Umbea
Huwezi kukuta mtu furaha akiwa mbea kwa sababu haoni sababu ya kuongea mambo ya watu wala kuyafatilia. Hivyo ukitaka furaha maishani, acha kufatilia mambo ya watu yasiokuhusu.
Kushikilia visasi
Huweiz kuwa na furaha kama una chuki na ugomvi na mtu yeyote ile kwani muda wote utakuwa unawaza ugomvi.