Mambo manne (4) ya kufanya kama hupati choo

HomeElimu

Mambo manne (4) ya kufanya kama hupati choo

1.Kunywa maji yakutosha
Unywaji wa maji mara kwa mara unapunguza uwezekano wa kupata tatizo la kushindwa kupata haja kubwa. Endapo umepata tatizo hilo tayari, ni vyema kutumia maji kwa wingi kuliko soda au juice.

2. Kula matunda na mbogamboga kwa wingi
Matunda husaidia uchafu (kinyesi) kusafiri vizuri kwenye utumbo hivyo kukurahishia kupata haja kubwa vizuri kabisa. Matunda na mbogamboga pia kulainisha kinyesi na kukiweka katika hali ambayo itakuwa ni rahisi kusafiri.

3. Ukimaliza kule tembea kidogo
Moja ya sababu ya chanzo cha kukosa choo ni mtu baada ya kumaliza kula chakula kisha kukaa sehemu moja. Ina shauriwa kwamba ukishamaliza kupata chakula na baada ya kupumzika kidogo ili chakula kishuke vizuri, ni vyema ukasimama na kutembea kidogo kunyoosha viungo. Hii itarahisisha zaidi mmeng’enyo wa chakula tumboni na pia kuandaa mazingira mazuri yakupatikana kwa haja kubwa kwa urahisi.

4. Kunywa Kahawa
Wanasayansi wamegundua kwamba unywaji wa kahawa unasaidia kupatikana kwa choo kikubwa kwa urahisi. Kawaha ina sifa ya kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na kufanya pia kinyesi kiwe laini hivyo kuondoa usumbufu wakati wa haja kubwa.

error: Content is protected !!