Mambo matano yanayoweza kukupata ukiwa na kitambi

HomeElimu

Mambo matano yanayoweza kukupata ukiwa na kitambi

Kitambi hutokana hutokana na mlundikano wa mafuta mwilini kutokana na ulaji wa vyakula vya mafuta kwa wingi. Kwa wanaume mafuta hutunza kwenye eneo la tumbo na wanawake mafuta hayo hutunzwa kwenye matiti, makalio na maeneo mengine ya tumbo. Kuwa na kitambi kwa maana ya ongezeko la mafuta mwilini inaweza kumletea mtu madhara mbalimbali.

Hizi hapa athari za vitambi:

1. Hupunguza uwezo wa kushiriki tendo la ndoa
Kuna kasumba za mtaani wanasema wanaume wembamba wanajua sana kuridhisha wanawake. Hii ni kweli kwa kiasi kikubwa kwani wanaume wengi wanene huchoka sana kwa shughuli ndogondogo. Pia mafuta mengi kwenye mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume hufanya uume uishiwe nguvu kabisa. Matibabu ya nguvu za kiume kwa watu waha ni kupunguza unene tu wala hakuna miujiza yeyote katika hili.

2. Kupunguza mvuto wa kimapenzi
Hii ni kwa wanaume na wanawake, kuna wanaume ambao hawapendi mwanamke ambaye anakitambi kwani wengi wanakuwa wanapoteza muonekano wao mzuri. Vivyo hivyo kwa wanawake hawapendi ni wachache sana wanaopenda wanaume wenye vitambi.

3. Ugumba kwa wanawake
Unene husababisha homoni za wanawake kutokua katika mfumo mzuri [unbalanced]. Pia wanawake hawa hupata sana kansa za mifuko ya uzazi yaani ‘fibroids’. Hali hii huweza kusababisha kutozaa kabisa. Ni vizuri kama unaona unashindwa kupambana na unene wako uzae mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

4. Vifo vya ghafla
Zipo tafiti kadha wa kadha zinazoonesha kwamba watu wengi ambao wamekufa ghafla, ni wenye uzito uliopitiliza>
Watu hao huweza kufa usingizini kwa sababu unene husababisha hali fulani iitwayo ‘sleep apnoea’ ambayo muhusika hushindwa kupumua kwa muda wakati amelala, hali ambayo huweza kusababisha kifo kabisa.

5. Kansa za aina mbalimbali
Unene hufanya mwili kushindwa kupambana na seli zinazosababisha kansa hivyo mtu hua kwenye hatari ya kupata kansa ya figo, kansa ya kizazi, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya maini, kansa ya tezi dume, kansa ya kongosho, kansa ya koo, kansa ya matiti, kansa ya mlango wa uzazi na nyingine nyingi.

Unene na kitambi sio kuridhika au asili tu ya mtu, hapana, Kuna uwezekano wa kupungua kwa asilimia mia moja kama ukiamua kupunguza unene na kuna uwezekano wa mtu mwembamba kuwa mnene, kwani vyote hivyo huchangiwa na aina ya maisha tunayoishi. Kikubwa ni kuwa makini katika mfumo wa lishe na mazoezi.

error: Content is protected !!