Mambo sita (6) ya kuzingatia kabla ya kusaini mkataba

HomeElimu

Mambo sita (6) ya kuzingatia kabla ya kusaini mkataba

Mkataba aua kandarasi ni makubaliano wanayoingia watu au taasisi katika kuongoza mahusiano au ushirika wao kweye jambo fulani. Kwa kusaini mkataba, unaonesha kukubaliana na yote yaliyopo katika mkataba huo ikiwa ni pamoja na adhabu unazoweza kukumbana nazo iwapo utakiuka masharti ya mkataba huo.

Kabla ya kusaini mkataba wowote, ni lazima uzingatie mambo haya saba;

1. Soma na kuelewa kila kilichomo

Usiingie kwenye mtego wa mazoea na kuamini kwamba maneno yanayotumika kwenye mikataba yote yanafanana. Wala usiwe mvivu kwa kusoma sehemu ndogo tu ya mkataba, hakikisha unasoma kila kitu na kukielewa.

2. Jipe muda wa kutosha

Usikurupuke, hata kama unahitaji sana kazi hiyo  usisaini mkataba kwa haraka. Unapopewa mkataba jipe muda ili uweze kusoma na kufanya maamuzi ya uhakika.

3. Tafuta ushauri au msaada wa wataalam

Huwezi kufahamu kila kitu. Hata kama wewe ni mtaalam wa kazi ambayo unaenda kuifanya baada ya kupata mkataba huo, ni vyema ukapata ushauri au msaada wa Wanasheria au watu wengine wanye ujuzi katika maeneo ya mbalimbali yanayohusiana na mkataba huo.

4. Fahamu haki na wajibu wako

Mkataba unahusisha kutoa na kupokea. Kutoa ni wajibu wako na kupokea ni haki yako. Fahamu unachotakiwa kutoa ili ufahamu kwa undani juu ya kile unachostahili kupokea.

5. Kila kitu kiwekwe kwenye maandishi

Usifanye makosa ya kuamini ‘mali kauli’ (maneno tu). Hakikisha yote unayoyataka yameandikwa kwenye mkataba.

6. Mkataba unatawaliwa na Sheria

Yote yaliyoandikwa kwenye mkataba yanayongozwa na sheria za nchi husika. Usifikiri kwamba mkataba unaweza kuwa jambo la kawaida tu au jambo la kirafiki ambalo unaweza kusaini lakini usilifuate.

Masharti yote lazim ayafuatwe na iwapo yatakiukwa adhabu zake zitatolewa kwa mujibu wa sheria.

 

 

error: Content is protected !!