Mambo sita ya kufanya kabla ya miaka 30

HomeElimu

Mambo sita ya kufanya kabla ya miaka 30

‘Siku hazigandi’, msemo wenye ukweli usiofichika aliowahi kuimba Lady Jaydee. Bila kujipanga siku, mwezi na mwaka vitaisha ukiwa unazidi kuongeza miaka bila kuona mafanikio katika maisha yako.

Kabla ya kufikisha miaka 30 ni vyema kuhakikisha umefanyia kazi yafuatayo;

Nidhamu ya pesa ni muhimu sana katika kufanikiwa kwenye yote unayofanya. Jifunze kusevu kiasi cha fedha kwaajili ya baadaye. Fanya manunuzi yako kwa kuangalia vitu unavyovihitaji zaidi ya unavyovitaka tu.

Vile vinavyoweza kuachwa viache na vinavyoweza kusubiri visubiri. Hakikisha unajipangia matumizi yako ya kila mwezi na kuweka kiasi cha ziada kwenye akaunti ya akiba.

Wajue ndugu na rafiki zako kwa ukaribu. Marafiki ni sehemu kubwa ya maisha yako, hivyo kabla ya kufikisha miaka 30 lazima uwe na marafiki unaojua utaenda nao mbali na ndio wakati wa kuachana na marafiki wanaokutoa kwenye reli ya malengo yako.

Ndugu nao ni wakati wa kujua namna ya kuishi nao. Fahamu tazia za ndugu zako, ni watu wa aina gani na ndugu wapi wa kukaa nao mbali na wapi wa kuwaweka karibu.

Tabia zile zinazokuwa kikwazo cha wewe kufanya vizuri kwenye majukumu yako ya kila siku, ziorodheshe. Kila mwaka acha tabia moja moja na kujitahidi kuanza tabia nyinginenzuri mpya kila mwaka.

Tandika kitanda chako kila siku asubuhi. Jenga tabia ya kuamka mapema na kutandika kitanda chako kabla ya kuondoka ndani. japo ni kidogo ila kufanya jambo la kwanza asubuhi kwa ukamilifu hasaidia kupunguza mawazo na kukusaidia kupangilia kazi zako vyema kila siku.

Jijengee tabia ya kujifunza kitu kipya kila mwaka. Angalia ni nini ungependa kujifunza na wapi unataka kunoa zaidi maarifa yako kisha anza kujifunza kitu hicho. Itakusaidia kupanua wigo wako wa kufikiri na kufanya na kufanya akili iwe active all the time.

Toa sadaka. Sio tu zaka ila pia kusaidia wahitaji. Chagua kimoja na ukifanya mara kwa mara ili kukujengea nidhamu ya kujali wengine na kujifunza kupitia maisha ya wengine. Iwe kutoa damu, kusaidia walemavu, wazee, yatima hata wasiojiweza. Tafuta jambo la kufanya kusaidia wengine.

error: Content is protected !!