Maoni ya wadau juu ya faragha ya taarifa mitandaoni

HomeKitaifa

Maoni ya wadau juu ya faragha ya taarifa mitandaoni

Baada ya kelele za kutaka kuwepo kwa sheria ya kulinda data nchini kuwa nyingi, wadau mbalimbali wametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kulinda faragha za watu kwenye mitandao na watumiaji wa bidhaa zinazohusiana na data.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya sheria hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu huku Naibu Katibu wa Wizara hiyo, Dkt Jim Yonazi akisema kuwa sheria hiyo mpya itamtaka mtu yeyote anayekusanya taarifa binafsi kuzilinda kwa mujibu wa sheria.

Mwanzilishi wa Jamii Forums, Maxence Mello ni mmoja wa wadau ambaye amekuwa akitetea uundwaji wa sheria ya ulinzi wa data na mwathirika wa kesi zinazohusiana na data, alipendekeza sheria hiyo iende sambamba na utaratibu mzuri wa udhibiti wa matumizi ya mtandao na taarifa binafsi.

“Tunahitaji mifumo inayofaa ya kukusanya data binafsi na kuhakikisha data zetu ziko salama. Pia , tunashauri kuundwa kwa chombo huru kitakachosimamia hili,” alisema Mello. Sheria zinazosimamia mawasiliano zinaelekeza watoa huduma za mawasiliano kulinda taarifa za wateja wao lakini endapo taarifa hizo zitahitajika kutumika kwenye kesi mahakamani na upepelezi basi kampuni hizo hukabidhi data hizo kwenye mamlaka husika kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

error: Content is protected !!