Mapacha wanaokula magodoro

HomeKitaifa

Mapacha wanaokula magodoro

Joyce Mrema mama wa mapacha wawili amejitokeza hadharani na kupaza sauti akiomba msaada wa madaktari bingwa,kujitosa kuwatibu wanawe wanaokula magodoro badala ya chakula.

Kwa mujibu wa mama huyo, watoto hao waliacha kula vyakula vya kawaida walipofikisha umri wa miaka mitatu na sasa wanakula magodoro jambo linalompa hofu mama huyo akihisi tatizo hilo linaweza kuwasababishia kuziba kwa utumbo.

“Nilishawahi kuwapeleka hospitali ndogo ya Levolosi, nikaambiwa wamekosa madini fulani. Nikashauriwa niende nyumba ya Mungu, Mwanga nikachukue dagaa niwachemshe na niwape wanywe na kuwachemshia ‘corn flower’ za kijani. Najaribu wapi wanakula magodoro tu,”alibainisha.

Joyce anasema, magodoro ndani yanaisha hali inayomlazimu kuwafungia nje anapokuwa ametoka au anapofanya shughuli zake nje ili kuwadhibiti.

Mama huyo anaomba msaada wa kwenda kwenye hospitali kubwa ili kuweza kupata suluhisho la tatizo hilo la watoto wake kwani akiwapikie chakula cha kawaida hawawezi kula na badala yake wanaenda kukitupa chooni na kisha kula magodoro.

Kwa mtu yoyote aliyeguswa kusaidia watoto hao wakapate matibabu watumie fedha zao kupitia namba za mama wa watoto hao 0763876313 jina Joyce Mrema

 

 

error: Content is protected !!