Rais Samia kununua magoli ya Simba SC na Yanga SC

HomeKitaifa

Rais Samia kununua magoli ya Simba SC na Yanga SC

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa Sh milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakati wa michuano inayoendelea ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewaeleza Wahariri jijini Dar es Salaam.

Simba itakutana na vinara wa Kundi C, Raja Casablanca katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Jumamosi Februari 18, 2023 wakati Yanga itaburuzana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Yanga na Simba zote zilianza vibaya katika michuano hiyo ya Shirikisho barani Afrika.

error: Content is protected !!