Mauzo ya nyama nje yapaa

HomeKitaifa

Mauzo ya nyama nje yapaa

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema ndani ya miezi sita mwaka huu Tanzania imeuza nyama tani 10,000 katika nchi za Bara la Asia na kuvunja rekodi ya mwaka jana.

Akifungua warsha ya siku saba ya wataalamu wa sekta ya mifugo kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, Waziri wa wizara hiyo, Mashimba Ndaki alisema ongezeko la mauzo ya nyama nje ya nchi ni matokeo ya ziara za Rais Samia Suluhu Hassan ughaibuni kuvuta wawekezaji.

Alisema hadi Desemba mwaka huu huenda Tanzania ikauza nyama nyingi zaidi kuliko miaka yote kwa kuwa mwaka jana iliuza nyama tani 7,000 tu.

Ndaki alisema wizara hiyo imeweka mpango kazi wa kuhakikisha wafugaji wanafuga mifugo bora ili kumpatia mlaji bidhaa bora kwa maslahi ya nchi.

Alisema wizara hiyo imepanga kuboresha sekta ya mifugo kwa kufuga kisasa katika vituo vya ng’ombe na mbuzi ili kuwe na mifugo bora kumudu ushindani sokoni kimataifa kwa maslahi ya nchi.

 

error: Content is protected !!