Waziri Ummy: Corona bado ipo

HomeKitaifa

Waziri Ummy: Corona bado ipo

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kuepuka kuambukizwa virusi vya corona vinavyosababishwa na ugonjwa wa Covid-19 kwani bado ni tishio nchini kutokana na kasi ndogo ya kuchanja.

Alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa majengo ya afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya CCBRT,mkoani Dar es Salaam.

Alisema wiki hii maambukizi zaidi yameripotiwa na asilimia kubwa ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam.

“Kuna maswali watu wengi wananiuliza kuhusu barakoa wakishangaa kwanini wazungu hawavai huku Watanzania wakisisitizwa kuendelea kuvaa.”

“Wale hawavai barakoa kwa kuwa wamechanja hadi kufikia wastani wa asilimia 70 ndio maana hawavai. Hata hapa kama tungechanja hadi kufikia asilimia 50, ningewatangazia watu wasivae barakoa, hivyo tuendelee kuchanja ili kufikia viwango vitakavyotuwezesha kuacha barakoa,” alisema Waziri Ummy.

 

error: Content is protected !!