Mtoto wa miaka 2 akatwa shingo na kutupwa

HomeKitaifa

Mtoto wa miaka 2 akatwa shingo na kutupwa

MTOTO wa miaka miwili, Nkeya Thomas ameuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kichakani katika Kijiji cha Nyamigogwa, Kata ya Shabaka wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Jamuhuri William juzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na wananchi wa Shabaka. Tukio hilo linadaiwa kutokea Juni 7 mwaka huu.

“Ndugu zangu wana Shabaka, najua na nyie hiki kitendo hamkikubali, waliokifanya kitendo hiki hawako mbali na sisi na kila mtu mwenye moyo wake, anahisi kwamba kuna mtu fulani ndio aliyehusika.

“Kwa sababu mtoto amechinjwa kabisa, nimemuona hapo, ninyi ndio wenyeji wa maeneo haya, tunaomba ushirikiano wenu, ili hawa waliohusika na kitendo hiki cha kinyama wapatikane wafikishwe mbele ya sheria.”

Akizungumza katika mazishi ya mtoto, Mama mzazi wa Nkeya anayefahamika kwa jina la Mperwa Sayari alisema alipata taarifa za mwili wa mwanae kuonekana umechinjwa na kutupwa wakati yeye akiwa msibani.

“Niliamka asubuhi nikawakorogea uji wakanywa, baada ya hapo nikaenda kilioni (msibani) saa nne asubuhi, ila ilipofika saa saba mchana nikarudi nyumbani kwa sababu nina mtoto mchanga.

error: Content is protected !!