Zanzibar ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza

HomeKitaifa

Zanzibar ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi akutana na kufanya mazungumzo na timu ya Masoko ya Klabu ya Southampton ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Wamefanya mazungumzo hayo kuangalia njia za kusaidia kuitangaza Zanzibar kiutalii kuipitia klabu hiyo katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Ujumbe huo wa Southampton FC uliongozwa na Mshauri Elekezi, Ammy Ninja na pia uliambatana na uongozi wa juu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale na Kamisheni ya Utalii Zanzibar.

error: Content is protected !!