Benki ya Standard Chartered Kenya imepunguza kiasi kikubwa cha hisa zake katika dhamana za serikali ya Kenya kwa 52% baada ya kupata hasara ya uwekezaji huo.
Hasara hiyo imefanya uwekezaji wake nchini Kenya kupungua hadi KSh 54 bilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2023 ikilinganishwa na KSh 111 bilioni mwaka jana.
Kupungua kwa kiasi hicho kikubwa ni hatari kwa serikali ya Kenya katika uchumi wake hasa wakati huu ambapo inakabiliwa na madeni.
Hatua hiyo imekuja wakati ambao wasiwasi umeongezeka wa kufilisika kwa baadhi ya mataifa ya Afrika ambayo yana mazingira magumu ya kiuchumi.