Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewaeleza na kuweka wazi waandishi wa habari mambo makuu matatu aliyozungumza na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka gerezani mwezi Machi tarehe 4, 2022.
“Waheshimiwa viongozi nilipokwenda kukutana na Mhe, Rais Ikulu tulichokizungumza ni kitu komoja tu cha msingi, kwamba tulikubaliana kutafuta njia za haki za mazungumzo za mashauriano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili taifa letu,
“La pili,. tulikubaliana tuache kuzungumza neno amani, amani, amani kila wakati tuzungumze haki, haki, haki kila wakati , kwamba tutakutanishwa kama taifa pale ambapo viongozi wataitanguliza haki katika kila hatua ya maisha yetu,
“La tatu nilimfahamisha Rais kwamba apende yeye ama apende yeyote, ukweli ni kwamba CHADEMA ni Chama kikuu cha upinzani nchini, na huwezi ukapuuza political process yoyote kwakuki exclude, kwakukiacha nje chma kikuu cha upinzani nchini haiwezekani,” alisema Freeman Mbowe.
Aidha, katika mazungumzo hayo na waandishi wa habari, Mbowe aliweka msimamo wa CHADEMA katika kuhudhuria vikao vya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa kusema kuwa agenda za vikao hivyo ni kusitisha mchakato wa kupata katiba mpya.
“Tumeangalia na kamati kuu nia gani iko nyuma ya TCD, hoja gani zinawakilishwa kwenye kikao cha TCD. Hapa hatuyaoni ufumbuzi wakupata katiba ya nchi yetu tunaona mkakati wakuhairisha agenda ya katiba kwa taifa hili, hatuwezi kuwa sehemu yake. Kwahiyo sio Mbowe wala kiongozi yoyote wa CHADEMA atashirki vikao hivyo,” alisema Mbowe.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alisema pia kuwa, hawezi kupata katiba mpya ya nchi wenyewe hivyo kusema wapo tayari kwa ajili ya mazungumzo na maridhiano na vyama vingine ili kuweza kufanikisha jambo hilo.