Meena Ally alia na kifo cha rapa RickyRic

HomeBurudani

Meena Ally alia na kifo cha rapa RickyRic

Mtangazaji wa redio ya Clouds kutoka nchini Tanzania, Meena Ally ameonyesha kuguswa na kifo cha rapa kutoka Afrika Kusini RickyRic aliyekutwa amefariki nyumbani kwake huku ikisemekana kwamba amejinyonga.

Meena ameandika kwamba inawezekana Ricky akawa amechukua maamuzi hayo kutokana na msongo wa mawazo kwa jinsi ambavyo watu walimsema siku ya wapendanao kwenye mtandao wa Twitter.

Ikumbukwe kwamba Meena aliwahi kupitia changamoto yakusemwa na kuandamwa kwenye mitandao ya kijamii na hivyo kueleza kwamba watu wengine hushindwa kustahimili maneno na matusi wanayopata hivyo kuchukua hatua ya kujitoa uhai.

Meena amewata watanzania na kila mtu duniani kuachana na vitendo hivi vya kusema watu kwenye mitandao ya kijamii kwani vinaweza kuleta madhara makubwa zaidi kwakuwa wengi hushinwa kustahimili hai au kukabiliana na hali hiyo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Meena Ally (@meena_ally)

error: Content is protected !!