Amazon imefunga rasmi jana Mach 17,2022 mkataba wake wakuinunua kampuni ya MGM kwa kiasi cha fedha dola bilioni 8.5 na kusema kwamba hakuna mfanyakazi wa MGM atakayeachwa nyuma wakiamiaanisha kwamba wataendelea kufanya kazi kama kawaida.
Amazon na MGM walitangaza kwamba MGM imejiunga na Prime Video na Amazon Studios. Studio hiyo yenye hadithi nyingi, iliyodumu kwa karne nyingi—iliyo na zaidi ya vichwa vya filamu 4,000 , vipindi 17,000 vya TV, Tuzo 180 za Academy, na Tuzo 100.
Makamu Mkuu wa Rais wa Prime video na Amazon Studios, Mike Hopkins alisema kwamba anayofuraha kuwakaribisha wafanya kazi wa MGM na kushirikiana nao kwenye tasnia ya sanaa.
“Tunakaribisha wafanyikazi wa MGM, waundaji, na talanta kwa Prime Video na Amazon Studios, na tunatazamia kufanya kazi pamoja ili kuunda fursa zaidi za kuwasilisha hadithi bora kwa wateja wetu.” alisema Hopkins.