‘Mgombea Urais’ Kenya aogopa kuibiwa na Wagombea wenzake

HomeKimataifa

‘Mgombea Urais’ Kenya aogopa kuibiwa na Wagombea wenzake

Gavana wa Machakos ambaye pia ameweka azma ya kugombea urasi nchini Kenya Dr. Alfred Mutua amesema kwamba hataki kuzungumzia kuhusu mipango na ilani yake ya uchaguzi kwa sasa kwani anahofia wapinzani wake wataiba mipango/ilani yake.

Mutua wakati akizungumza na kituo cha runinga cha Citizen amesema kuwa hafurahishwi na ahadi ambazo amekuwa akizisikia kutoka kwa wapinzani wenzake, kwani ni ahadi ambazo hazina mustakabali mwema katika kulikomboa Taifa la Kenya kiuchumi. “Ahadi zao hazituhakikishii namna kulipa deni la Taifa wala namna ya kukidhi mahitaji yetu” Alisema Mutua.

Mutua ameongeza atakuja na ilani ambayo itakuwa Mwarobaini wa matatizo ya Kenya na asingependa kuizungumzia kwa sasa kwani wataiba mawazo yake. Mwezi uliopita Mutua alisema kuwa ameunda kamati ambayo ilifanya utafiti na kuja majibu kwamba kwa sasa yeye ana nafasi kubwa ya kushinda uraisi nchini Kenya, huku Kiongozi wa ODM Raila Odinga na mwezie wa UDA William Ruto akiwaacha kwa mbali sana.

error: Content is protected !!