Mitandao ya kijamii chanzo ya magojwa ya akili, kichaa

HomeUncategorized

Mitandao ya kijamii chanzo ya magojwa ya akili, kichaa

Tatizo la afya ya akili nchini limeongezeka kwa 40% huku wataalam wa afya wakiainisha kuwa takwimu kwa sasa zinaonesha kwenye kila watu wanne, mtu mmoja ana tatizo la afya akili ambapo lisipotibiwa kwa wakati huweza kusababisha mtu kupata kichaa.

Wagonjwa waliokuwepo mpaka mwaka 2020 ni 500,000, kutoka wagonjwa 357,799 mwaka 2018.

Ugonjwa wa afya ya akili husababishwa na msongo wa mawazo, matumizi ya dawa za kulevya na vilevi lakini kwa sasa unachangiwa zaidi na mitandao ya jamii ambapo waathirika wakubwa ni vijana kwani wamejikuta wakitamani kuwa na maisha wanayoyaona kupitia mitandao hiyo.

        > Uonapo dalili hizi, jua anataka kujiua

Kuna dalili ambazo mtu mwenye tatizo la afya ya akili anakuwa nazo ni kama kutoa lugha mbaya kwa watu wengine mara kwa mara au namna anavyotoa maoni yake mtandaoni lazima akosee wengine, upokeaji wake wa jambo ni wa makasiriko muda wote.

Mbali na kupata kichaa, ugonjwa wa akili usipotibiwa athari zake ni pamoja na kupata shinikizo la damu, kupoteza hamu ya kula, kuzalishwa zaidi kwa homoni za hasira, kupata msongo wa mawazo na kupata mabadiliko kwenye mzunguko wa damu.

Ugonjwa wa akili unatibika, ni muhimu kwa jamii kukubaliana na tatizo na kutafuta tiba badala ya kuendelea kuishi na tatizo hilo.

error: Content is protected !!