Polisi wa Afrika Kusini wameanzisha msako wa kuwasaka washukiwa walioiba mkanda wa ndondi uliotolewa kwa Nelson Mandela na bingwa wa Marekani Sugar Ray Leonard.
Mkanda wa ubingwa wa ndondi aliopewa Nelson Mandela na bondia maarufu Sugar Ray Leonard umeibiwa kwenye jumba la makumbusho nchini Afrika Kusini, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo.
Wafanyikazi waliofika kazini kwenye jumba la makumbusho asubuhi waligundua kuwa kufuli zilikuwa zimechezewa, na wakaingia ndani na kugundua mkanda huo haupo kwenye Nyumba ya Mandela huko Orlando Magharibi, Soweto, chombo cha habari cha Afrika Kusini TimesLIVE kiliripoti.
Sugar Ray Leonard alimpatia Mandela mkanda huo muda mchache baada ya kutoka jela mwaka 1990.