Rais Samia atoa msamaha kwa wadaiwa kodi ya ardhi

HomeKitaifa

Rais Samia atoa msamaha kwa wadaiwa kodi ya ardhi

Serikali imetangaza masamaha wa kodi kwa wadaiwa sugu wa ardhi zikiwemo taasisi za dini na mashirika kulipa madeni yao bila riba katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

Msamaha huo ni kuanzia Julai hadi Desemba mwaka huu ambapo umelenga watu ambao wanadaiwa katika kipindi kisichozidi miaka mitano.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema taasisi zinazoongoza kwa kudaiwa madeni ya muda mrefu ni pamoja na  taasisi za dini na kuwataka  viongozi wa madhehebu hayo kuhakikisha wanatumia fursa ya msamaha huo kulipa.

“Najua kuna wengi wanadaiwa madeni ya muda mrefu kwa hiyo kumetokea msamaha kuanzia mwezi julai mpaka desemba mwaka huu, watakaoweza kulipa ndani ya miezi hii sita, wale ambao madeni yao yana miaka mitano kurudi nyuma watalipa bila ile tozo ya riba” alisema Dkta Mabula.

” Mhe mama Samia ameridhia kupitia waziri wa fedha kwa kushirikiana na waziri wa ardhi waweke utaratibu mzuri wa ninyi kuondolewa tozo ile na msamaha ni wa miezi sita tu kama una ndugu mpigie simu mwambie serikali ya awamu ya sita chini ya mama samia imetoa msamaha kwa wadiwa sugu ili watoke katika jina baya la wadaiwa sugu kwenda kulipa madeni bila riba” alisema Dkt Mabula.

Waziri Mabula amewataka wenye maeneo  yaliyochukuliwa kama ya umma lakini yanasoma majina ya watu binafisi kufanya marekebisho mara moja kwakuwa serikali haitakubaliana kuona migogoro inayotokea baina ya waumini na viongozi wa dini.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, mmiliki wa ardhi atakayeshindwa kulipa madeni yake katika kipindi cha miezi hiyo sita basi atadaiwa madeni yake pamoja na riba na akishindwa kufanya hivyo atafikishwa kwenye vyombo vya sheria ambako huko uamuzi wake ni kulipa ama kunyang’anywa ardhi anayoimiliki.

 

 

error: Content is protected !!