Mkuu wa Mkoa Geita aagiza V8 ya Mkurugenzi itumike kubeba wagonjwa

HomeKitaifa

Mkuu wa Mkoa Geita aagiza V8 ya Mkurugenzi itumike kubeba wagonjwa

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, ameagiza gari la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, aina ya Toyota Land Cruiser V8, litumike kubebea wagonjwa wanaohitaji rufaa katika Kituo cha Afya Muganza baada ya gari la wagonjwa kuharibika matairi.

Mnyeti ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda, lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato, baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu kusimama kwa huduma ya gari la wagonjwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Mnyeti amekemea hali hiyo akisema haikubaliki huduma muhimu ya kuokoa maisha kusimama kwa sababu ya matairi, akieleza kuwa changamoto hiyo ilipaswa kutatuliwa na uongozi wa halmashauri bila kusubiri ziara.

error: Content is protected !!