Winga wa Yanga, Bernard Morrison amelimwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda ambaye alikuwa ameanguka chini wakati wa harakati za kugombea mpira.
Morrison alifanya kosa hilo, mechi iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapana kifungo kilichotumika kumuadhibu ni kanuni ya 42:5 (5.6) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji, ambapo hatacheza dhidi ya Ruvu Shooting, Namungo FC na Simba.
Wakati Morrison akipata adhabu hiyo, waamuzi waliyosimamia mchezo huo (Yanga vs Azam), Ahmed Aragija, mwamuzi msaidizi namba moja Frank Komba kutoka mkoa wa Dra es Salaam, wamepelekwa kwenye kamati ya waamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa ajili ya kujadiliwa baada ya kushindwa kuumudu vyema mchezo huo.