Katika kuhakikisha wateja wanapata uhakika wa kutumia huduma za mawasiliano, Kampuni ya Halotel Tanzania imeahidi kuwekeza zaidi katika kuboresha ubora wa miundombinu ya mtandao ili kuongeza kasi ya 4G.
Abdallah Salumu, Mkurungenzi wa Kituo cha Biashara cha Halotel alisema kwamba kampuni hiyo imeongeza wigo wa mtandao takribani nchi nzima na kufikia asilimia 95 ya Watanzania.
“Katika miaka miwili ijayo tutawekeza zaidi kwenye miundombinu ili kuhakikisha huduma bora za mawasiliano ili kuongeza ubora wa huduma,”
“Kampuni inaendelea kutandaza minara ya 4G katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo huduma hizo hazijawahi kuwapo awali. Lengo ni kuwa na wateja wengi walioboresha nambari yao ya 3G hadi 4G,”alisema Salumu.
Aidha, kwa mujibu wa Salumu, hadi kufikia sasa wamesambaza minara 800 ya mawasiliano ya kizazi cha nne katika kipindi cha miaka sita ili kueneza mawasiliano ya kidigitali kote nchini.