Mtuhumiwa aachiwa baada ya muathirika kukataa kubakwa

HomeKitaifa

Mtuhumiwa aachiwa baada ya muathirika kukataa kubakwa

Mahakama ya Mkoa Wete imelionoda shauri la kubaka lililokuwa linamkabili mtuhumiwa Omar Hemed Abdi (23) mkazi wa Kwake Micheweni baada ya mtoto wa miaka 12 aliyedaiwa kufanyiwa kitendo hicho kukana.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Omar Ali Abraham alisema analiondoa shauri hilo chini cha kifungu cha 103 (a) cha sheria nambari 7 ya mwaka 2018.

“Mahakama hii baada ya kupata ushahidi huo, imeamua kuiondoa kesi iliyokuwa ikimkabili mtuhumiwa Omar Hemed Abdi, kutokana na mtoto mwenyewe kusema kuwa hakufanyiwa kitendo hicho na mtuhumiwa ,” alisema hakimu huyo.

Awali ilidaiwa mahamani hapo kuwa, Februari 3 mwaka 2021 majira ya saa 8:00 usiku katika kijiji cha Kwale Micheweni, Omar Hemed Abdi alidaiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye miaka 12 mkazi wa Kwale Micheweni jambo ambalo ni kosa kisheria.

error: Content is protected !!