Mrema kuzikwa Alhamisi Agosti 25,2022 Moshi

HomeKitaifa

Mrema kuzikwa Alhamisi Agosti 25,2022 Moshi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP,Agustino Mrema anatarajiwa kuzikwa Alhamisi Agosti 25 katika kijiji cha Kilalacha mkoani Kilimanjaro.

Maziko hayo yatatanguliwa na ibada ya mazishi siku ya Jumatano itakayofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Salasala kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Agosti 22,2022 na mwanaye, Michael Mrema wakati akitoa ratiba ya msiba.

 

error: Content is protected !!