Msuya ataka katiba ipatikane haraka

HomeKitaifa

Msuya ataka katiba ipatikane haraka

Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya ameishauri Serikali kufikiria na kuona namna ya kufunga mjadala wa kupatikana Katiba mpya ili watu wajenge taifa badala ya kuendelea kusikia jambo hilo kila siku.

Amesema hayo jana Jumanne Julai 19 2022, baada ya kuwasilisha maoni yake mbele ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa na kusema kuwa kama kutakuwa na taarifa mpya za kuongezwa basi ifanyike hivyo Katiba ipatikane.

“Katiba Mpya nimesema ni vizuri tukafika mwisho ‘tuifinallize’ kwa mazungumzo yote yaliyofanyika na kama kuna habari mpya waongeze, tupate hiyo Katiba na baada ya hapo watu tufanye kazi tusiwe kila mwaka tunakaa tunarudia Katiba,” amesema Msuya.

Aliongeza kwa kushauri kuwa asilimia kubwa ya wananchi ni vijana, hivyo kikosi kazi kifikirie suala la kutoa elimu ya uraia mwema kwa vijana kwa mifumo mbalimbali ili kuwajenga Watanzania wa rika la kesho watakaofanana na wazee wazalendo waliopo sasa.

Msuya (91) aliwahi kuwa Waziri Mkuu mwaka 1980 hadi 1983 na baadaye Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka 1994 hadi 1995.

Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni Katibu Mkuu katika wizara mbalimbali na Waziri katika wizara za fedha(1970-1975) na 1993 hadi 1989), Viwanda (1975-1980) na Viwanda na iashara mwaka 1990 hadi 1994.

error: Content is protected !!