Mtanzania ‘Geay’ aweka  rekodi Boston Marathon

HomeKimataifa

Mtanzania ‘Geay’ aweka rekodi Boston Marathon

Mwanariadha Gabriel Geay, anayeiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya mbio kitaifa ameshika nafasi ya nne katika mbio za Boston Marathon zilizofanyika Boston, Marekani.

Geay ametumia saa 2:07:53 kumaliza mbio hizo huku mshidi wa kwanza, Evans Chebet akimaliza mbio kwa saa 2:06:51.

Ingawa Geay amepanda daraja, ametumia muda mrefu zaidi ya kipindi cha nyuma alipovunja rekodi ya Tanzania kwa kutumia saa 2:04:55 kwenye mbio Milano na kuweza kufuzu kushiriki ‘2020 Tokyo Olympic Games.’

Peres Jepchirchir kutoka Kenya, aliyeshika nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya 2020 Tokyo Olympics kwa kumaliza ndani ya saa 2:27:20, aliibuka pia mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake, ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki Boston Marathon.

Jepchirchir alimaliza mbio ndani ya saa 2:21:01 ikiwa ni mapema zaidi ya muda aliotumia Tokyo.

 

 

error: Content is protected !!