Sababu ya Mwl. Nyerere kutaka kuacha urais 1980

HomeKitaifa

Sababu ya Mwl. Nyerere kutaka kuacha urais 1980

Wakati wa Kongamano la kumbukizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mtoto wake Charles Makongoro Nyerere ameelezea namna baba yake alizungumza naye kwa kina kwanini alitamani kuachia uongozi ifikapo 1980.

Ingawa mpango wake huo haukufanikiwa na Nyerere kustaafu 1985, moja ya sababu za kutaka kustaafu mapema ni kuweza kuona namna kiongozi anayemfuta atakavyoongoza nchi.

“Wakati anafanya hayo maamuzi kwamba nataka nikapumzike wakati afya yangu bado nzuri, pia nipate muda nione hata rais mmoja wakwangu [Mtanzania] anavyoongoza,” amesema Makongoro.

Baba wa Taifa alifanikiwa kuona uongozi wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Hayati Benjamin Mkapa.

error: Content is protected !!