Mtanzania mwingine auawa nchini Israeli

HomeKitaifa

Mtanzania mwingine auawa nchini Israeli

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema amejulishwa na Serikali ya Israel kwamba kijana wa Kitanzania, Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel ameuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba 2023.

BBC News Africa on X: "Boarding a plance was an exciting moment for  Tanzanian Joshua Mollel. His trip to Israel was the first time he travelled  abroad. In early October, his new

Kupitia taarifa ya waziri huyo inaeleza Serikali ilifanya jitihada kubwa ya kumtafuta kijana huyo ambaye ilipoteza naye mawasiliano tangu tarehe 7 Oktoba 2023.

“Tumejulishwa na Serikali ya Israel kwamba Joshua Mollel, kijana wa Kitanzania aliyekuwa anasoma nchini Israel, na ambaye tulipoteza naye mawasiliano tangu tarehe 7 Oktoba 2023, na ambaye Serikali imekuwa inafanya jitihada kubwa kupata taarifa zake tangu wakati huo, aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba 2023.

“Nimeongea na Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo wa Serikali ya Israel.” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza

“Tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada.

“Kwa ridhaa ya familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo.”

error: Content is protected !!