Mtoto auzwa kwa milioni 1 kukabili njaa

HomeKimataifa

Mtoto auzwa kwa milioni 1 kukabili njaa

Taifa la Afghanistan linapitia kipindi kigumu tangu wanamgambo wa Kiislamu wa Taliban kufanya mapinduzi ya Kijeshi Agosti mwaka huu. Nchi za Magharibi zilizokuwa zikipeleka misaada ya kibidamu nchini humo zimeshitisha misaada hiyo kwa muda na kuacha watu wengi kwenye baa la njaa.

Nje kidogo ya mji wa Herat, familia moja yenye watoto wa wanne, wakiume wakubwa watatu na wa mwisho wa kike, imechukua uamuzi mgumu wa kuuza mtoto mchanga ili wapate fedha ya kulisha watoto wengine wasipoteze maisha kwa njaa. Mama wa Kichanga hicho akiongea kwa uchungu amesema, “Siwezi kuona watoto wangu wanakufa wote, inaniuma sana kumuuza binti yangu, lakini nimefanya hivyo kuokoa wengine.”

Baba wa kichanga hicho kazi yake kubwa ni kukusanya takataka, lakini hali ilivyo sasa hata kazi hiyo imekuwa ngumu kupatikana.

      > Fahamu mbinu inayotumika kumtambua rafiki wa kweli kwenye mafanikio

“Hatuna unga wala mafuta, hatuna chochote, ilitulazimu kumuuza binti yetu. Sijui akiwa mkubwa atanifikiriaje, lakini imetulazimu kufanya hivyo.”

Mtu aliyemnunua mtoto huyo ambaye wasifu wake haukuwekwa wazi, amekubaliana na familia hiyo kwamba atamtwaa mtoto huyo rasmi kutoka kwa familia yake pindi atakapoanza kutembea.

Mnunuzi huyo ametoa zaidi ya milioni moja kwenye manunuzi ya mtoto huyo ili isaidie familia miezi kadhaa mbele, huku familia ikiwa na imani pengine hali itatengemaa.  Mnunuzi ameongeza kuwa, binti huyo atakapokua mkubwa ataolewa na mtoto wake wa kiume.

Hali ni mbaya katika eneo hilo, kwani si familia hiyo pekee iliyouza mtoto wao, watoto kadhaa wameshauzwa na watu wenye fedha.

error: Content is protected !!