Jarida la The Sun la nchini Uingereza limeripoti kuwa katika Hospitali ya watoto ya Albert Sabin katika mji wa Fortaleza nchini Brazil amezaliwa mtoto mwenye mkia wenye urefu wa sentimeta 4. Mkia huo wa ajabu wa kushangaza unaoonekana kuvimba mwishoni kwenye ncha na wenye umbo la duara.
Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miezi nane, kabla ya kuzaliwa vipimo havikuonyesha kama kulikuwa na shida ya yoyote mpaka mzazi wake alipomzaa ndipo iligundulika kuwa mtoto amezaliwa na mkia.
Mkia huo unaonekana kuumbwa kwa kwa tishu zenye mafuta na kiinitete pamoja na tishu tishu zisizo na mfupa, Mkia huo bado haujulikana kama ulikua unasababisha maumivu kwa mtoto ama haukua unampa maumivu.
Daktari kutoka nchi hiyo anasema ni kawaida binadamu wote huwa na mkia ila unaingia ndani wiki chache baada ya ujazito, na ni nadra sana kukuta mtoto amezaliwa akiwa na mkia, Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mtoto wa kwanza kuzaliwa akiwa na mkia ilikua ni zamani kwenye karne ya 19.